to love | kupenda |
I love you. | Ninapenda wewe. |
He loves seagulls. | Anapenda shakwe. |
Do you like tea and coffee? | Je unapenda chai na kahawa ? |
I don't like you. | Sipendi wewe. |
They don't like to eat fish. | Hawapendi kula samaki. |
to swim | kuogelea |
I like to swim. | Ninapenda kuogelea. |
I swim in the sea. | Ninaogelea baharini. |
The fish swims in the sea. | Samaki anaogelea baharini. |
The fishes swim in the sea. | Samaki wanaogelea baharini. |
My cat doesn't swim. | Paka wangu haogelei. |
My cat doesn't like water. | Paka wangu hapendi maji. |
to be afraid of | kuogopa |
My cat is afraid of water. | Paka wangu anaogopa maji. |
You (pl) are afraid of crocodiles. | Ninyi mnaogopa mamba. |
The elephant is not afraid of crocodiles. | Tembo haogopi mamba. |
to walk | kutembea |
We are walking on the sand. | Tunatembea juu ya mchanga. |
also / too | pia |
We are also walking on the rocks. | Tunatembea pia juu ya mwamba. |
to fly / jump | kuruka |
Birds fly. | Ndege wanaruka. |
Are you jumping? | Unaruka? |
No, I am not jumping. | Hapana, siruki. |
The people are afraid and jump. | Watu wanaogopa na wanaruka. |
to live | kuishi |
in / inside | katika |
I live in a house. | Mimi ninaishi katika nyumba. |
I live at home. | Mimi ninaishi nyumbani. |
I don't live in the sea. | Siishi baharini. |
to be | kuwa |
I am not. | Si |
I am not a fish. | Mimi si samaki. |
We are not fishes. We don't live in the sea. | Sisi si samaki. Sisi hatuishi baharini. |
You are a lion. | Wewe ni simba. |
to eat | kula |
They eat fish. | Wanakula samaki. |
They don't eat snails. | Hawali konokono. |
Sharks eat littie fishes. | Papa wanakula samaki wadogo. |
Sharks don't drink coffee. | Papa hawanywi kahawa. |
to have | kuwa na |
I have a cat. I don't have dogs. | Nina paka. Sina mbwa. |
I am a cat. I am not a dog. | Mimi ni paka. Mimi si mbwa. |
I will be a cat. | Nitakuwa paka. |
I will have a cat. | Nitakuwa na paka. |
When I am big... (when I grow up...) | Nikiwa mkubwa |
If I eat vegetables, I will get big. | Nikila mboga, nitakuwa mkubwa. |
If I eat I, I will drink, too. | Nikila, nitakunywa pia. |
If I eat fish, I will drink water. | Nikila samaki, nitakunywa maji. |
to go | kwenda |
When you go to the sea, you will walk on the sand. | Ukienda baharini, utatembea juu ya mchanga. |
When we go to the sea, we will swim. | Tukienda baharini, tutaogelea. |
When you swim in the sea, you will be afraid of sharks. | Ukiogelea baharini, utaogopa papa. |
to hunt | kuwinda |
If he hunts a shark, he will eat this shark. | Akiwinda papa, atakula papa huyu. |
everything | kila kitu |
If they like lobster, they will eat everything. | Wakipenda kambakoche, watakula kila kitu. |
When the seagulls fly over the sea they will hunt for fish and crabs. | Shakwe wakiruka juu ya bahari, watawinda samaki na kaa. |
The dolphin jumps out of the water. | Pomboo anaruka nje ya maji. |
When the dolphins swim in the sea, they also jump out of the water. | Pomboo wakiogelea baharini, pia wataruka nje ya maji. |
When the seagulls hunt for crabs, they also hunt for sea snails. | Shakwe wakiwinda kaa, pia watawinda konokono wa baharini. |
If people eat lobsters, they also like oysters. | Watu wakikula kambakoche, pia watapenda chaza. |